27 Desemba 2025 - 14:46
Israel imekubali kuitambua Somaliland kwa masharti ya kukubali kuwapokea wakazi wa Gaza!

Jana, Benjamin Netanyahu, Gideon Sa’ar Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni, pamoja na Abdirahman Mohamed Abdullahi, rais wa kujitangaza wa Somaliland, walitia saini tamko la pamoja la kuitambua Somaliland kama nchi huru na inayojitegemea.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- siku moja baada ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, kutangaza kuitambua Somaliland kama nchi huru, Kituo cha Televisheni cha Israel Channel 14 kilitangaza kuwa Tel Aviv imekubali kuitambua Somaliland kama nchi huru kwa masharti ya eneo hilo kukubali kuwapokea wakazi wa Gaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Russia Today (Russia Al-Youm), kituo hicho kiliongeza kuwa tamko la kuitambua Somaliland, lililoandaliwa kwa misingi ya Makubaliano ya Abraham, linajumuisha kuanzishwa kwa mahusiano kamili ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kimkakati katika nyanja mbalimbali. Aidha, Somaliland kwa malipo ya kutambuliwa kwake, itawapa makazi sehemu ya wakazi wa Gaza katika ardhi yake.

Jana, Benjamin Netanyahu, Gideon Sa’ar Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, na Abdirahman Mohamed Abdullahi, rais wa kujitangaza wa Somaliland, walitia saini tamko la pamoja la kuitambua Somaliland kama nchi huru.

Netanyahu pia alimualika Abdullahi kufanya ziara katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Gideon Sa’ar, baada ya mazungumzo yake na Abdullahi, alitangaza kuwa uhusiano kati ya pande hizo mbili uliimarishwa katika mwaka uliopita kupitia mawasiliano ya mara kwa mara, na leo tumetia saini makubaliano ya kutambuana na kuanzisha mahusiano kamili ya kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa mabalozi na kufunguliwa kwa balozi.

Utawala wa Kizayuni, pamoja na ushirikiano wa kiusalama na kisiasa na Somaliland, una nia ya kupanua ushirikiano huo hadi katika sekta kama kilimo, teknolojia, biashara na afya.

Mwitikio kuhusu hatua ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Somalia

Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia, katika kujibu hatua hii ya utawala wa Kizayuni, ilitangaza kuwa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia ni nchi moja, huru na isiyogawanyika, na hatua yoyote inayokiuka ukweli huu inachukuliwa kuwa “batili na isiyo na uhalali wa kisheria”.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar pia ilieleza kuwa kuitambua eneo la “Somaliland” na utawala wa Kizayuni ni mfano hatari na ni kitendo kinachokwenda kinyume na sheria za kimataifa, na kinachochukuliwa kama uvamizi dhidi ya mamlaka na umoja wa ardhi ya Somalia.

Katika taarifa hiyo, serikali ya Qatar ilisisitiza kupinga vikali uamuzi wa Israel wa kuitambua “Somaliland”.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar iliongeza kusisitiza kuwa inapinga juhudi zozote za kuunda au kulazimisha mamlaka sambamba zinazodhoofisha umoja wa Somalia.

Ikumbukwe kuwa eneo la Somaliland liko katika bara la Afrika, katika pwani ya kusini ya Ghuba ya Aden. Kaskazini-magharibi linapakana na Djibouti, na kusini pamoja na magharibi linapakana na Ethiopia.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha